TICD ARUSHA: UCHAGUZI WA RAISI NA MAKAMU WAKE WAPAMBA MOTO.
Wanafunzi wa chuo cha taifa cha maendeeo ya jamii alimaarufu kama TICD Tengeru juzi siku ya jumatatu wamejitokeza kwa pamoja kushiriki kikamilifu kumchagua raisi na makamu wa serikali ya wanafunzi ijuikanayo kama TICD-SO.
Katika zoezi hilo bwana KINGU D. KINGU alijitokeza kuwania kiti cha uraisi wa chuo hiki bila kuwepo kwa mgombea mwenza na bwana ISMAIL MASSAWANGA  naye alijitokeza kuwania kiti cha makamu wa raisi bila kuwepo kwa mgombea mwenza.
Bwana KINGU D INGU alishinda na kutangazwa kupata kura za NDIYO  asilimia 66% nae ISMAIL MASSAWANGA alipata asilimia 72% za kura za ndiyo, hivyo kufanya bwana KINGU D KINGU kuwa raisi wa serikali ya wanafunzi wa TICD SO pamoja na bwana ISMAIL MASSAWANGA kuwa makamu wa raisi wa TICD-SO.

Na Castory Mbunda,
blogger




Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog